Makubaliano ya Huduma
1. Utangulizi
Jiongeze Fintech Company Limited (Jiongeze Fintech) inakukaribisha kutumia Jiongeze App (Application) application inayowakutanisha wauzaji wa bidhaa (Muuzaji/Wauzaji), wanunuzi (Watumiaji/Mtumiaji/Mnunuzi) na watoa huduma za mikopo (Mkopeshaji/Wakopeshaji) na kuweza kufanya bishara kwa urahisi. Jiongeze App imekusudia kuwawezesha watumiaji wake kupata bidhaa mbalimbali kwa kuwapa njia zaidi ya moja ya kuzilipia kulingana na vipato na uwezo walionao, lengo likiwa ni kumuwezesha kila mmoja kuweza kupata kitendea kazi au kifaa anachokihitaji kwa uwezo wake wa kukilipia bila kujiumiza yeye binafsi au biashara yake.
Makubaliano haya yameandaliwa ili kuifanya Jiongeze App ifikie malengo yake katika kutoa huduma bora, lakini pia kukuwezesha wewe mtumiaji wake kufikia malengo yako uliyoyakusudia. Hivyo basi, kwa kuendelea kutumia Application ya Jiongeze utakuwa umekubali kuingia mkataba huu wa huduma kati yako na Jiongeze Fintech, vinginevyo tafadhali usiendelee kutumia Application ya Jiongeze.
2. Wajibu wa Wako (Mtumiaji)
Ili kuwa mtumiaji wa Jiongeze App, yakupasa:
- Kuwa na umri usiopungua miaka 18 na mwenye akili timamu.
- Kujisajili kwa kutumia taarifa za kweli, ikiwa ni pamoja na majina kamili, nambari ya simu iliyosajiliwa kwa jina lako, pamoja na anuani ya makazi.
- Kuto kutoa au kutuma One Time Password (OTP) yako kwa mtu yoyote pamoja na wafanyakazi wa Jiongeze.
- Kulinda taarifa za akaunti yako ilikuhepuka wizi wa taarifa zako na matumizi mabaya.
- Kutoa taarifa za wauzaji wasio waaminifu na wanaokiuka utaratibu.
- Kutoa taarifa za mtu yoyote mwenye nia ya kutumia Jiongeze App kijume na makubaliano haya.
- Kukubali kwa hiari yako kufuata matakwa ya makubaliano yaliyoainishwa katika ukurasa huu.
3. Bidhaa
- Bidhaa методыzote zinazowekwa na zitakazowekwa Jiongeze App ni mali ya Wauzaji.
- Wauzaji ndio wanaopanga bei, maelezo pamoja na picha, na kuuza bidhaa.
- Ni wajibu wako kama mtumiaji kuhakikisha unapewa bidhaa yenye ubora na utakayoridhika nayo kutoka kwa muuzaji pamoja.
- Wauzaji wana haki ya kubadilisha bei za bidhaa kwasababu mbalimbali ikiwemo za kiuchumi.
- Wajib wako kudai risiti halali (EFD) ya malipo na warranty.
- Jiongeze haitahusika endapo utashindwa kutekeleza majukumu yako kama mnunuzi.
- Toa taarifa za Muuzaji atakiuka wajibu wake, unayo haki ya kutoa taarifa ya ukiukwaji huo ili kwa pamoja tushirikiane kuukomesha.
4. Manunuzi na Malipo
- Utaruhusiwa kununua bidhaa zaidi ya moja kwa mara moja.
- Malipo yote bidhaa yanafanyika ndani ya Application ya Jiongeze.
- Kwa kufanya manunuzi umeipa Jiongeze ruhusa ya kutoa taarifa zako binafasi (Jina lako, namba ya simu, na anuani yako) kwa Muuzaji.
- Muuzaji anaweza kutoza malipo mengine nje ya bei ya bidha, kama gharama za usafirishaji).
- Jiongeze haitahusika na malipo yaliyofanywa nje ya Application.
- Toa taarifa Jiongeze ikiwa umeombwa kufanya malipo ya bidhaa nje ya utaratibu.
- Unaweza kununua bidhaa kupitia Jiongeze App kwa (a) kulipia taratibu kwa awamu (b) Kwa mkopo kutoka kwa wakopeshaji.
- Bidhaa ikibadilishwa bei, bei mpya itaowahusu na watu ambao hawajamaliza malipo ya bidhaa wanazonunua kwa awamu.
- Ikiwa bidhaa uliyokuwa unanunua imeisha kwa muuzaji, una haki ya kuomba kurudishiwa pesa yako yote.
5. Mkopo
- Unayo haki ya kuomba mkopo.
- Jiongeze haitoi mikopo, bali inafanya kazi na taasisi zilizosajiliwa kisheria kutoa mikopo nchini.
- Ukiomba mkopo, ombi lako litatumwa kwa mkopeshaji atakayekuwepo.
- Unahaki ya kuchagua taasi ya kutuma ombi lako la mkopo.
- Kwa kutuma ombi la mkopo, utakuwa umeipa ruhusu Jiongeze kutoa taarifa zako binafsi kwa taasi ya kutoa mikopo.
- Mkopeshaji ana haki ya kukubali au kukataa ombi la mkopo.
- Makubaliano ya mkopo yatakuwa ni kati yako na taasisi itakayotoa mkopo.
- Maombi yote ya mikopo yatakayopitia Jiongeze yatakuwa ni kwa ajili ya kulipia bidhaa. Sio pesa taslimu.
- Vigezo na masharti ya mikopo pamoja na gharama vitawekwa na mkopeshaji.
- Jiongeze haitakusanya malipo ya marejesho ya mikopo.
6. Taarifa Binafsi
Jiongeze App inakusanya taarifa za zako (mtumiaji), ikiwa ni pamoja na jina, nambari ya simu, anwani ya makazi, jinsia na taarifa za miamala ya malipo na matumizi ya App. Matumizi ya taarifa hizi ni pamoja na:
- Kukuhudumia kwa urahisi na ufanisi.
- Kuboresha huduma.
- Kutoa taarifa zinazohusu miamala na huduma zetu, na.
- Kuwasiliana nawe.
- Kutimiza matakwa ya kisheria Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
7. Haki Miliki
Haki miliki za bidhaa, bei, picha, nembo, na maelezo mengine yanayohusiana na bidhaa ni mali ya wauzaji au watoa mikopo washirika. Nembo ya Jiongeze, alama, maudhui, Application na mfumo ni mali ya Jiongeze. Hauna haki ya kutumia rasilimali hizi kwa madhumuni ya kibiashara bila ruhusa ya maandishi kutoka kwa wamiliki. Jiongeze haitawajibika kwa ukiukaji wowote wa haki miliki unaofanywa na mtumiaji.
8. Marufuku
Ni marufuku kutumia Jiongeze App kwa madhumuni yoyote yasiyo halali, na yaliyo kinyume malengo yake ikiwa ni pamoja na:
- Kutakatisha fedha.
- Kudanganya au kutapeli wengine.
- Kuwa na akaunti zaidi ya moja.
- Kutumia Jiongeze kuvunja sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Ukiukaji wa marufuku hizi utasababisha kufutwa kwa akaunti na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yako ikiwemo kufunguliwa mashitaka mahakamani.
9. Kufungwa kwa Akaunti
Jiongeze ina haki ya kufunga Akaunti yako wakati wowote bila kukupa taarifa, zifuatazo zinaweza kuwa sababu za akaunti yako kufungwa:
- Ukikiuka vigezo na makubaliano yaliyowekwa hapa.
- Tuekeleza agizo halali kutoka katika mamlaka za dola na za kisheria sheria.
- Endapo utaomba kufunga akaunti yako.
10. Haki za Mtumiaji
Kama Mtumiaji una haki zifuatazo:
- Kujisajili na kufungua akaunti bure kwa kuzingatia makubaliano haya.
- Kununua bidhaa yoyote.
- Kuchagua njia na muda wa kufanya malipo.
- Kuomba mkopo kwa watoa huduma za mikopo.
- Kusitisha ununuzi wake na kurudishiwa pesa zilizolipwa.
- Kuomba taarifa zake za kibinafsi zifutwe, kwa kuzingatia sheria za Tanzania zinazohusu uhifadhi wa taarifa za miamala ya kifedha.
- Kuomba kupakua taarifa zake binafsi.
- Kufuta taarifa zake binafsi.
- Kupewa taarifa zinazohusu mabadiliko katika utoaji wa huduma.
11. Ada Zinazochajiwa
Jiongeze inaweza kutoza ada za huduma kwa mtumiaji, kama ilivyoelezwa kwenye jukwaa. Ada hizi zinaweza kujumuisha:
- Ada za miamala kwa ununuzi wa bidhaa.
- Ada za kusindikiza malipo kwa awamu au mikopo (kama zipo). Mtumiaji ataarifiwa mapema kuhusu ada zozote zinazohusika.
- 5% ya kiasi kilicholipwa itakatwa kama ada ya kusitisha manunuzi katika.
12. Mabadiliko ya Vigezo na Masharti
Jiongeze App ina haki ya kubadilisha Makubaliano haya wakati wowote. Mtumiaji ataarifiwa kupitia ujumbe mfupi wa Maneno, notisi kwenye App, au mawasiliano mengine yanayofaa. Kuendelea kutumia App baada ya mabadiliko ni kukubali kama kukubali Makubaliano mapya.
13. Mawasiliano
Kwa maswali, malalamiko, au maoni kuhusu Jiongeze App, unaweza kuwasiliana nasi kupitia:
- Nambari ya Whatsapp: +255 685833429
- Instagram/ X/ Tiktok/ Facebook: @JiongezeApp
- Barua pepe: support@jiongeze.co.tz
- Tovuti: www.jiongeze.co.tz
Tutajitahidi kukujibu haraka iwezekanavyo ndani ya masaa 24 kwa swala la kawaida na masaa 48-72 kwa swala lenye uzito.
Timiza Ndoto kwa #MalipoYasiyoumiza - Download Jiongeze App.